
Hayawi hayawi sasa ya mekuwa, Tanzania to lagos Nigeria, hili ni tukio la kihistoria ,siku isio weza kusaulika kwa mashabiki na wadau wote wa tasnia ya sanaa hususani mziki ...
Tukio la kukata na shoka , Sherehe ya harusi ya wanandoa super star Juma Jux , na mtoto mkali kutoka nchini Nigeria mke halali Priscilla ilifanyika usiku wa tarehe 28 May 2025 ,ndani ya ukumbi wa kimataifa maarufu "Superdome" Masaki. Hakika ilikuwa ni sherehe ya aina yake ambayo imejaza watu ikiwemo mastar wakubwa wa ndani na njee ya nchi.
Diamond platnumz, zuchu, Nandy na mumewe Billnass, S2kizzy na wengine kibao wameonekana kwenye tukui hili wakiwa na nyuso za furaha huku pia wakiwa wamevalia mavazi ya aina yake yani watu waliulamba na kupendeza sana,huku mziki ukitawala wakati wageni walikwa wakila na kunywa wakisherekea.
Wanandoa hao Jux na mkewe Priscilla wamakuwa ni mfano wa kuigwa baada ya watu kuja na maswali kwa wasanii wengine wata funga ndoa lini ? Akiwemo star Diamond Simba, hivyo pia kwa wasanii wa kike pia wataolewa lini??
kupitia mitandao yetu ya kijamii instagram na facebook @stbongo ,Unaweza tupa maoni yako juu ya sherehe hii ya ndoa ya Jux na Priscilla ,pia muonekano wa star gani umekuvutia zaidi?
MPIGA PICHA WETU @MR LEVO ST BONGO DIGITAL
Ungana nasi kupitia kisumbuzi @startimestz CH 161 (antena) CH 401 (Dish) pamoja na kwenye YouTube channel yetu ya #STBongoTV Kwa Taarifa zaidi.