MAKONDA AMKABIDHI RC MPYA ARUSHA ,AMTAKA ANDELEZE NDOTO YA KUUFANYA MAKAO MAKUU YA EAC

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amemuomba Mkuu wa Mkoa mpya, Kenani Kihongosi, kuhakikisha anaendeleza ndoto ya kuufanya Mkoa wa Arusha kuwa na hadhi ya Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).


 Repoter : ‎Gladness Kowero, Arusha

‎Makonda alitoa kauli hiyo wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika jijini Arusha, ambapo alieleza kuwa ana imani na uongozi wa Kihongosi kuwa ataendeleza mipango na maono aliyoyaacha.

‎“Ninaamini kuwa Kihongosi ataendeleza yale yote tuliyoyaanzisha, hususani dhamira ya kulifanya Jiji la Arusha kuwa mfano wa Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,” amesema Makonda.


‎Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa mpya, Kenani Kihongosi, aliahidi kushirikiana na wananchi na viongozi mbalimbali kuhakikisha kuwa huduma kwa jamii hazikwamishwi kwa namna yoyote ile.


‎ “Nitaendeleza pale alipoishia aliyenitangulia. Lengo ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bila vikwazo,” amesema Kihongosi.

Share: