
Hutuba na zoezi kubwa la kuweka Jiwe la Msingi ,Limejenga historia mkoani Simiyu, Mhe.Dkt, Samia huku akikabithiwa Tunzo kutoka kwa Waziri wa maji ,mradi wa kukabiliana na mabadiliko na tabianchi uko tayari,fahamu zaidi hapa,
Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi ni mpango maalum unaolenga kupunguza madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa na kusaidia jamii kuhimili athari zake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya shukrani kutoka kwa Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuwahutubia wananchi wa Nyashimo, Busega mkoani Simiyu tarehe 19 Juni, 2025.
Mradi huu una tambulika kwa jina la Mradi Simiyu "Endelevu", ni Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kwa Maendeleo Shirikishi”. Mkoa wa Simiyu (wilaya kama Bariadi, Meatu, Maswa, Itilima na Busega) ndipo mahali pa utekelezaji wa mradi huo wenye Lengo kuu la Kuwezesha jamii ya Simiyu kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia uhifadhi wa mazingira, matumizi ya nishati mbadala, na kilimo kinachostahimili hali ya hewa.
Simiyu Endelevu ni Mradi mkubwa ambao utafanyika ndani ya muda wa Miaka Mitatu, huku ukiwa na malengo mengine mengi yakiwemo Kuelimisha jamii juu ya mabadiliko ya tabianchi na mbinu za kukabiliana nayo,Kuongeza upandaji wa miti na kurejesha maeneo yaliyoharibiwa,Kukuza matumizi ya nishati mbadala kama majiko banifu na sola,Kuwajengea uwezo wakulima kutumia mbinu bora za kilimo hifadhi,Kuanzisha mifumo ya tahadhari yaapema dhidi ya ukame na mafuriko.
Kaya maskini vijijini (hasa wanawake na vijana),Vikundi vya wakulima na wafugaji,Shule, vituo vya afya na taasisi za kijamii ndio walengwa mahususi wa mradi huu mkoani Simiyu. Kampeni za uhamasishaji: vipindi redio, warsha, mabangoUpandaji miti: miti milioni 1 ndani ya miaka 3,Usambazaji wa majiko banifu kwa kaya 5,000,Mafunzo ya kilimo hifadhi na matumizi ya mbegu zinazostahimili ukame,Uwekaji wa paneli za sola kwa shule 50 na zahanati 20,Uanzishaji wa vikundi vya mazingira kwa vijana mashuleni hizo ndio shughuli kuu za Mradi wa Simiyu " Endelevu".
Matarajiwo makubwa kwa wananchi wakiongozwa na serekali ya Ccm, Tanzania inayo ongozwa na Rais mchapakazi na mwenye Utu na kupitia Mradi huu utakuwa na mafanikio / matokeo haya Uelewa wa mabadiliko ya tabianchi kuongezeka kwa zaidi ya 80% ya wakazi,Kupungua kwa matumizi ya kuni na mkaa kwa 50%,Uzalishaji wa mazao kuongezeka kwa 30% kwa kutumia kilimo hifadhi,Hifadhi ya misitu na mito kuongezeka kutokana na upandaji miti,Jamii kuwa na uwezo wa kukabiliana na majanga kama ukame na mafuriko.
Tufuatilie kupitia #STBongoTV ndani ya kisimbuzi cha @startimestz CH 161 (antena) CH 401 (Dish) pamoja na kwenye YouTube channel yetu ya #STBongoTV Kwa Taarifa zaidi.