
Amakweli kazi nikwako! Kauli mbiu ilio zoeleka na kushika atamu inaendelea kuishi kwa vitendo ndani ya Vodacom kwenda kwenye sekta ya elimu nchini Tanzania kidigital ni uwekezaji wa ma bilioni ambao unategemea kuleta tija na mabadiliko makubwa..
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Mitaala katika Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE), Dkt. Angela Katabaro (kushoto), na Mkurugenzi wa Mahusiano wa Vodacom na Vodacom Tanzania Foundation, Zuweina Farah (kulia), wakishiriki katika hafla ya utiaji saini wa ishara kwa niaba ya taasisi zao kwa ajili ya ushirikiano wa kuviwezesha Vituo 184 vya Rasilimali za Walimu kwa vifaa vya TEHAMA na intaneti ili kusaidia mafunzo ya walimu kupitia mpango wa MEWAKA. Hafla hii imefanyika leo katika Hoteli ya Mount Meru, Arusha wakati wa uzinduzi rasmi wa Wiki ya CSO 2025.
Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza East Africa, Bi. Anna Bwana (kushoto), na Mkurugenzi wa Mahusiano wa Vodacom na Vodacom Tanzania Foundation, Zuweina Farah (kulia), wakionyesha makubaliano ya ishara ya ushirikiano wao unaotarajiwa kupanua mpango wa KiuFunza Pay-by-Skill unaolenga kuboresha elimu ya msingi. Tukio hili limefanyika leo katika Hoteli ya Mount Meru, Arusha wakati wa Wiki ya CSO 2025.
Kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE), Vodacomitaviwezesha Vituo 184 vya Rasilimali za Walimu (TRCs) kwavifaa vya TEHAMA na huduma ya intaneti ya uhakika ilikusaidia utekelezaji wa mpango wa serikali wa Maendeleo Endelevu ya Utaalamu wa Walimu (TCPD) ujulikanao kamaMEWAKA. Miundombinu hii ya kidijitali itawawezesha walimuzaidi ya 300,000 nchini kote kufikia vifaa vya kujifunza kupitiaMfumo wa Usimamizi wa Kujifunza (LMS), na hivyokuboresha ubora wa ufundishaji kwa mujibu wa mtaala mpyawa msingi wa umahiri wa mwaka 2023 wa Tanzania.
Dkt. Angela Katabaro, Mkurugenzi Mkuu wa TIE, alisema:“Uwezeshaji wa walimu kwa TEHAMA ni jambo la msingikatika utoaji wa elimu bora. Kupitia ushirikiano na Vodacom,tunaweza kupanua mpango wetu wa MEWAKA na kuzibapengo la kidijitali.”