
Temilade Openiyi, maarufu kama Tems, ni msanii wa Nigeria anayeandika, kutunga na kutayarisha muziki. Alianza safari yake ya muziki akiwa na umri mdogo, akijifunza kutunga nyimbo na kutayarisha muziki akiwa nchini Afrika Kusini. Alijulikana zaidi baada ya kuachia single yake ya kwanza, Mr Rebel, mwaka 2018. Mwaka 2019, alizindua single nyingine maarufu, Try Me, ambayo ilimjengea umaarufu zaidi. Alikuwa na kazi ya ofisi kabla ya kujitosa kikamilifu kwenye muziki mwaka 2018...
Tems alijulikana kimataifa baada ya kushirikishwa na Wizkid katika wimbo maarufu Essence mwaka 2020, ambao ulifikia nafasi ya 9 kwenye chati ya Billboard Hot 100 na kumletea umaarufu mkubwa. Alikuwa pia sehemu ya remix ya wimbo huo na Justin Bieber. Mwaka 2021, alishirikishwa na Drake katika wimbo Fountains, na mwaka 2022, sauti yake ilitumika kwenye wimbo Wait for U wa Future, akishirikiana na Drake.
Tems kuandika historia kwa kutumbuiza katika onyesho la kwanza la mapumziko ya nusu ya mechi kwenye mashindano ya FIFA.