RAIS MSEVENI KUWANIA TENA URAIS MWAKA 2026

Hizi sio tetesi tena, chama tawala National Resistance Movement nchini Uganda kimetoa tarifa yenye uthibitisho na kwa tarifa zaidi soma hapa...

Chama tawala nchini Uganda, National Resistance Movement (NRM), kimethibitisha kuwa Rais Yoweri Museveni atawania tena urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mapema mwaka 2026.


Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya chama hicho, Museveni “ameonyesha nia ya kuendelea kuwa mwenyekiti wa NRM na mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho kwenye uchaguzi wa 2026.” Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ndani ya NRM, Tanga Odoi, amethibitisha kwa shirika la habari la AFP kwamba Museveni atatangaza rasmi nia yake ya kugombea tena.



Museveni, ambaye sasa ana umri wa miaka 80, amekuwa madarakani tangu 1986, na licha ya kuwepo kwa tetesi, sasa ni rasmi kuwa anataka kuongeza muda wake wa utawala ambao tayari umefikia karibu miongo minne.

Share: