CRISTIANO RONALDO AMVISHA PETE MCHUMBA AKE BAADA YA MIAKA 9 YA MAHUSIANO

Baada ya mahusiano ya Miaka 9 Nguli wa soka na Binadamu mwenye wafuasi wengi zaidi Duniani kwenye mitandao ya kijamii Cristiano Ronaldo hatimae Siku ya jana alitangaza rasmi Kumchumbia mpenzi wake wa muda mrefu, Georgina Rodríguez.

Mbali na taarifa hiyo kuchukua vichwa vya habari duniani jingine ambalo limebeba uzito wa Uchumba huo ni pete Almas ambayo Ronaldo amemvalisha mpenzi wake ,kutajwa kuwa na thamani kati ya $2 million - $5 million (sawa na billion 5 mpaka 12 za Kitanzania).

Tufuatilie kupitia #STBongoTV ndani ya kisimbuzi cha @startimestz CH 161 (antena) CH 401 (Dish) pamoja na kwenye YouTube channel yetu ya #STBongoTV Kwa Taarifa zaidi.


#STBongoUPDATES #nyumbanikwanza

Share: