NAFASI YA SITA AMESHIKA RAY VANNY KATIKA "A" LIST YA WASANII WANAO SIKILIZWA ZAIDI AFRIKA

Rayvanny ameandika historia mpya kwenye YouTube Music baada ya kufikisha wasikilizaji milioni 34.1 wa mwezi, ndani ya siku tisa na kuwa msanii anayesikilizwa zaidi @youtubemusictanzania!.

Mafanikio haya yamechochewa na wimbo wake “Oh Mama Tetema”, aliomshirikisha Norah Fatehi, Vishal Mishra, na Shreya Goshal, ambao umewekwa kwenye chaneli kubwa ya muziki duniani T-Series yenye zaidi ya subscribers milioni 300. Ndani ya siku tisa pekee, video hiyo imewafikia zaidi ya watazamaji milioni 16, jambo lililoongeza kwa kasi namba za Rayvanny.


Wimbo wake wa 2019, “Tetema” alioshirikiana na Diamond Platnumz umeendelea kunufaika, ukivuka jumla ya wasikilizaji milioni 100 kwenye YouTube.


Kwa hatua hii, Rayvanny anabaki kuwa msanii pekee wa Afrika Mashariki aliyeingia kwenye Top 10 ya Afrika wenye wasikilizaji wengi wa mwezi Agosti kwenye YouTube Music, akithibitisha ushawishi wake katika kuhakikisha muziki wa Bongo Fleva unafika viwango vya kimataifa.


Share: