MISS WORLD NA MISS  WORLD AFRICA  WAMEWTEMBELEA KIWANDA CHA KUZALISHA TUMAINI KITS , ZMBF

Afisa Mtendaji Mkuu wa ZMBF, Bi. Fatma Fungo, amepokea ugeni maalum kutoka kwa Miss World na Miss World Africa, waliotembelea kiwanda cha uzalishaji wa Tumaini Kits kilichopo Migombani, Unguja.

Katika ziara hiyo, wageni hao mashuhuri walijionea kwa karibu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) kupitia Tumaini Initiative, kuhakikisha kila msichana balehe anabaki shuleni bila vikwazo vinavyotokana na changamoto za hedhi. Kupitia mradi huu, zaidi ya wasichana 9,000 kutoka skuli mbalimbali Unguja na Pemba wamepatiwa.


Miss World amepongeza jitihada hizi za ZMBF na kusisitiza umuhimu wa uwekezaji katika afya, elimu na ustawi wa mtoto wa kike kama nyenzo ya kujenga jamii imara na yenye usawa wa kijinsia.


Share: