ANANIA JR KATIBU MKUU MPYA CHA CHA MUZIKI WA DANSI TANZANIA (CHAMUDATA

Anania Junior anaingia katika historia kuwa Katibu Mkuu mdogo tangu kuanzishwa kwa Chama hiki cha Muziki wa Dansi nchini mwaka 1986.

Mtangazaji wa Tv kutoka @stbongotv ambae pia Mtoto wa Promoter Mkongwe Africa Mashariki na Mchezaji nyota wa zamani wa Timu za Yanga na Simba Sc Marehemu Anania Sangur, Anania Jr @anania_junior ameshinda nafasi ya Katibu Mkuu kupitia uchaguzi mkuu wa Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (Chamudata).

Anania Junior ni Mtoto wa Promoter Mkongwe wa Muziki wa Dansi Africa Mashariki Marehemu Anania Sangura ambae alifungua Milango ya Soko la Kimataifa la Muziki wa Dansi nchini kwa kuwaleta Wanamuziki Nyota kutoka Congo DRC akiwemo Pepe Kalle, Sam Mangwana, Madiluu, Mayaula, Soukous Stars, Awilo Longomba nk. Pia Anania Sangura alikuwa Nyota wa zamani wa Soka wa Simba na Yanga katika Miaka 1984 


Aidha Anania Junior ameshawahi kuwa Manager wa Wasanii kupitia THT mwaka 2017. Aidha Mwaka 2019 - 2020 amewahi kuwa Msaidi wa Meya wa Jiji la Dar Es Salaam (PR) Mhe. Abdallah Mtinika, pia amefanya kazi na Wasanii mbali mbali kama Ali Choki, Christian Bella, Papii Kocha, Tukuyu Sound Claudia Bakisa kutoka Congo DRC pia Mwaka 2022 aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano na Mitandao ya Kijamii Town Classic Band.


Chama Cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA)

Ni chama muhimu kabisa kinachowakilisha bendi za muziki wa dansi nchini Tanzania. Chama hiki kinaanzisha, kukuza na kulinda bendi zinazopiga muziki wa dansi (dans i), mtindo unaojumuisha rumba, soukous, na kwa kiasi kidogo kidumbaki na taarab. Muundo wake umejengwa tangu enzi za utawala wa kikoloni.

Mwaka 2016, CHAMUDATA ilifanya uchaguzi mkuu Dar es Salaam: Juma Ubao “King Makusa” alipata nafasi ya mwenyekiti, huku Lt Col Mwandike akisifika kama makamu mwenyekiti na Anna Mwaole kama katibu msaidizi.

Hivi sasa kuna Shirikisho la Muziki Tanzania lililoanzishwa mwaka 2021, linalojumuisha vyama mbalimbali vya muziki nchini. CHAMUDATA ni mojawapo ya vyama vinavyoshiriki ndani ya shirikisho hili. Kazi zake ni pamoja na kulinda maslahi ya wanamuziki, kukuza ushirikiano ndani ya sekta na kutoa ushauri wa kivitendo kwa wanachama wake.

Muziki wa dansi, au soukous / Tanzanian rumba, ulianzishwa nje kidogo ya enzi ya ukoloni katikati ya miaka ya 1930 jijini Dar es Salaam. Una sifa ya vionjo vya kiswahili, gitaa, ngoma, mabaki ya brass na sauti zilizofungwa pamoja kwa lengo la kuamsha wachezaji.

Bendi maarufu ndani ya muziki wa dansi ni pamoja na DDC Mlimani Park Orchestra, International Orchestra Safari Sound, Juwata Jazz, na Maquis Original. DDC Mlimani Park Orchestra, hasa, imekuwa kitovu cha mtindo huu tangu 1978.

Share: